Jumamosi 7 Februari 2026 - 12:00
Hukumu za kisheria | Kiwango cha kawaida cha matumizi ya mke (nafaqah)

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amejibu istiftaa (swali la kifiqhi) kuhusu “kiasi cha matumizi ya mke na khumsi yake”.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, moja ya masuala muhimu zaidi ya kifedha katika maisha ya ndoa ni matumizi ya mke (nafaqah) ambayo ni wajibu juu ya mume. Suala hili linaweza kuibua maswali kwa wanandoa wengi, hasa mwanzoni mwa maisha ya ndoa. Miongoni mwa maswali hayo ni kiwango cha matumizi ya lazima na pia hukumu ya khumsi yake. Katika muktadha huu, Ayatullah udhma Sayyid Ali Khamenei amejibu maswali mawili muhimu kuhusu matumizi ya mke na khumsi yake, ambayo yanawasilishwa kwenu kama ifuatavyo.

Swali:
1. Matumizi ya mke ambayo ni wajibu juu ya mume ni kiasi gani?
2. Je, matumizi anayopokea mke kutoka kwa mumewe yakibaki hadi mwisho wa mwaka wa khumsi inawajibika kutolewa khumsi?

Jawabu:
1. Matumizi ya lazima ya mke ni kila kitu ambacho kwa kawaida mke anahitaji, kama chakula na mahitaji yanayohusiana nacho, mavazi, makazi, gharama za matibabu ya magonjwa ya kawaida, usafi na mengineyo — kwa kiwango na ubora unaolingana na hali ya watu wa aina yake.

2. Matumizi (nafaqah) hayana khumsi, ingawa kwa tahadhari ya mustahabu, ikiwa yatabaki zaidi ya matumizi ya mwaka, ni vyema khumsi yake ilipwe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha